May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hashim Rungwe afunga mwaka na kilio cha katiba mpya

Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chaumma

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi wa Umma (Chaumma), Hashim Rungwe, amesema mwaka 2021 unaisha pasina kilio cha wananchi juu ya upatikanaji katiba mpya, kupatiwa ufumbuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Rungwe ametoa kauli hiyo leo Ijumaa, tarehe 31 Desemba 2021, jijini Dar es Salaam, akitoa salamu za kuufunga mwaka huo.

Mwanasiasa huyo amewataka Watanzania waendelee kushikamana, ili katiba mpya ipatikane.

“Watanzania kwa ujumla, naomba muendelee kufanya uvumilivu na kuwa tulivu wakati tunapambana kuhakikisha hii katiba tunakwenda kui-amend (rekebisha) vizuri, ili iweze kukidhi mahitaji ya wananchi. Ni katiba ambayo watu wa CCM wenyewe wameitunga wanaingia kuzuia,” amesema Rungwe.

Mwenyekiti huyo wa Chaumma amesema, Watanzania wanataka marekebisho ya katiba, ili kuondoa mapungufu yaliyomo katika katiba iliyopo.

“ Sisi tunataka katiba ambayo wananchi wote watakuwa wanaitegemea, sisi wote tutakuwa binding kwenye katiba tuzungumze tufanye mambo yetu. Katiba yetu iwe nzuri na iwe na muelekeo, sio mtu mmoja amezidi juu ya ile katiba, yeye ndiye ana power (nguvu) zaidi hapana,” amesema Rungwe.

Rais Samia Suluhu Hassan

Rungwe amesema “sisi wote tegemeo ni katiba, ambayo itatukutanisha kwa pamoja. Itaondoa matabaka, katiba hii inatujengea matabaka, huyu ndio huyu. Sio sasa tukienda namna hiyo tutakuwa hatufiki na tunaleta kichefu chefu kwa watu wengi duniani, wanaona hawa Watanzania vipi hata ueleweki.”

Mwanasiasa huyo amesema kuwa, mataifa mengi yamerekebisha katiba zake, ili ziendane na matakwa ya mazingira ya sasa.

“Nchi zote zinazotunzunguka wamevuruga katiba zao, wameshazi-amend. Wameshabadilisha utawala, sasa tawala hii tu ndiyo inang’ang’ania palepale, kwa kweli Watanzania tuendelee kushikamana ili tuweze kupata katiba mpya itakayotuletea umoja nakuondoa mvurugano uliopo,” amesema Rungwe.

error: Content is protected !!