August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Harufu yatawala Urusi Vs Uturuki

Recep Tayyip Erdogan, Rais wa Uturuki

Spread the love

HOFU ya kuvunjika kwa uhusiano baina ya Urusi na Uturuki imetanda kutokana na kuuawa kwa Andrei Gennadyevich Karloz, Balozi wa Urusi aliyekuwa kwenye jumba la maonesho ya picha jijini Ankara, anaandika Wolfram Mwalongo.

Karloz ameuawa jana ambapo mtuhumniwa wa shambulio hilo kwa mjibu wa video zinazosambaa mitandaoni, ni kijana mwenye jazba.

Kijana huyo alivaa suti nyeusi, shati jeupe na tai nyeusi akiwa na pisto, ameonekana akiwa ndani ya jengo hilo huku akitoa maneno makali, anadaiwa kufanya shambulizi la kushtukiza kwa kumpiga risasi balozi mgongoni.

Maria Zakharova, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi amethibitisha kifo cha balozi huyo ambapo amesema, ugaidi hauwezi kuisha lakini wataongeza nguvu katika kupamba nao “ugaidi hauwezi kuisha, tutapambana kwa nguvu zote.”

Vladimir Putin, Rais wa Urusi amesema tukio hilo ni hila za taifa hilo katika kukwamisha jitihada za kurejesha amani nchini Syria ambapo wapiganaji wa kikudi kutoka Uturuki wanatajwa kuhusika moja kwa moja katika njama za kutaka kumwondoa Rais Bashar Al Assad wa Syria.

“Uhalifu umeshafanyika, bila shaka hizi ni njama za kutaka kutaisha mahusiano yetu na Uturuki lakini yote hii inatokana na harakati za kulipatia amani taifa la Syria ambapo Urusi ndio iko mstari wa mbele katika kutimiza azma hiyo…, ni lazima tufahamu nani aliyepanga mauaji haya,” amesema Rais Putin.

Putin ameagiza Shirika la Upelelezi nchini mwake (FSB) kwenda nchini Uturuki kusaidiana na Shirika la Upepelezi la nchi hiyo (MIT) ili kumpata muhusika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua.

Receip Teyyip Erdogan, Rais wa Uturuki ameagiza vyombo vya usalama nchini mwake kubaini tukio hilo ambapo ametoia wito kwa mashirika mbalimbali kusaidia, huku akiruhusu Urusi kuingiza vyombo vya ulinzi ili kushirikiana naye.

Hata hivyo, taarifa za viongozi hawa wakuu (Putin na Erdogan) zimeonesha kuelekeana kutokana na rais huyo wa Uturuki kusema shambulio hilo linalenga kufifisha uhusiano wa mataifa hayo mawili lakini viongozi wote wameonesha ustahilimilivu wa hali ya juu hadi sasa.

Urusi imekuwa mwathirika mkubwa wa matukio ya kuuawa kwa Mabalozi wake hususan katika mataifa ya nayo kabiriwa na mapigano ya kundi linalo jiita Dola la kiislamu (IS).

Mwaka 1829, Balozi wa Urusi nchini Iran aliuawa kwa tukio la aina hiyo kitendo kinacho lifanya taifa hilo hasimu wa Marekani kujizatiti na makundi hayo kwa silaha za Nyuklia.

error: Content is protected !!