Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Harmonize kuwakutanisha jukwaa moja wasanii 50 wa Afrika Mashariki Dar
BurudikaHabari

Harmonize kuwakutanisha jukwaa moja wasanii 50 wa Afrika Mashariki Dar

Spread the love

 

WASANII zaidi ya 50 kutoka Afrika Mashariki wanatarajiwa kupanda jukwaa moja kwenye tamasha la ‘Afro East Carnival’ litakalofanyika Uwanja wa Tabata Shule, jijini Dar es Salaam tarehe 5 Machi 2022. Anaripoti Matlida Buguye…(endelea).

Tamasha hilo limeandaliwa na msanii wa muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Rajab Abdul maarufu Harmonize.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa, tarehe 11 Februari 2022 jijini Dar es Salaam, Harmonize amesema, tamasha hilo limelenga kuwaburudisha mashabiki wa muziki kwa kuunganisha ladha ya muziki wa Afrika ya mashariki.

Amesema, mpaka sasa tayari wasanii kutoka Afrika Mashariki watakaopanda jukwaani wamefikia 43 huku lengo likiwa kufikia wasanii zaidi ya 50.

Msanii huyo amegusia suala la wanii wenzake kutoka Tanzania, Jux na Darassa ambao wameonekana kutokubaliana na kuwajumuisha kwenye tamasha hilo pasina kuwauliza akisema, suala hilo linaendelea kufanyiwa kazi.

“Kila kitu kitakuwa sawa mameneja watakaa watazungumza itakuwa faraja kwangu kuwaona kaka zangu wanashiriki kwenye hili tamasha kwani nimeshirikiana nao kwenye kazi mbalimbali mfano kama darassa, ningeomba mnisamehe kwa kutoelewana kwenye hili,” amesema Harmonize

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!