May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Harmonize akanusha kumnyang’anya Country Boy gari

Spread the love

MKALI wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul ‘Harmonize’ na uongozi mzima wa rekodi lebo ya Konde Gang sio kweli kwamba walimpokonya msanii Country Boy gari bali alilirejesha mwenyewe.

Harmonize ametoa kauli hiyo hivi karibuni baada ya kuibuka uvumi kuwa gari alilokuwa akilitumia Country Boy kipindi akiwa chini ya lebo hiyo amenyang’anywa baada ya kuitosa.

Akizungumza katika kituo kimoja nchini Tanzania, Harmonize alifunguka kwamba Country Wizzy kabla ya muziki walikuwa ni washikaji wakubwa na ambao mwisho wa siku walikubaliana kuandikishiana mkataba kufanya kazi na Konde Gang.

Harmonize alisema kwamba msanii huyo ndiye aliridhia kurudisha gari tu kwa sababu alitambua kwamba wapo vijana wengine ambao wanaweza kuwa na uhitaji wa matumizi ya gari hilo pale Konde Gang.

error: Content is protected !!