September 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Harmonize ajiandaa kuitikisa Dar

Spread the love

Msanii wa Bongo fleva, Rajab Abdul maarufu kama ‘Harmonize’ ametangaza ujio wa tamasha lake katika jiji la Dar es salaam liitwalo (Afro East Carnival). Anaripoti Matilda Buguye…(endelea)

Tamasha hilo la Afro East Carnival litafanyika tarehe 5 Machi 2022 katika uwanja wa Tabata shule jijini Dar es salaam.

Aidha kupitia ukurasa wake wa instagram leo tarehe 8 Februari 2022, Harmonize ametangaza rasmi idadi ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo.

Idadi hiyo imejumuisha wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwemo Marioo, Ibraah, Moni centrozone, Otile brown, Eddy kenzo, Bruce Melodie, Dullah Makabila, Mabantu na wengine wengi.

Aidha, Hamornize ameweka bei ya kiingilio kwa mashabiki zake wa hali zote kuanzia 5000 na kuendelea.

error: Content is protected !!