Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Maisha Elimu Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi
Elimu

Harambee ujenzi sekondari za Musoma Vijijini yashika kasi

Spread the love

 

HARAMBEE ya ujenzi na ukarabati wa shule za sekondari zilizoko katika Jimbo la Musoma Vijijini, mkoani Mara, imeshika kasi baada ya Kampuni ya Nguvu Moja Security Services, kuchangia fedha kiasi cha Sh. 3.5 milioni kwa ajili ya ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi ya Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, fedha hizo zimewasilishwa jimboni humo na mwakilishi wa kampuni hiyo, Afisa wa Polisi Mstaafu, ASP Moyo.

Taarifa hiyo inasema kuwa, makabidhiano hayo yalifanyika katika duka la kuuzia vifaa vya ujenzi na kushuhudiwa na Prof. Muhongo.

Taarifa imesema kuwa, sehemu ya fedha hizo zimetumika kununua mifuko ya saruji 153, ambayo imesambazwa katika shule tatu za sekondari za Seka, Bwahi na Muhoji.

Jimbo la Musoma Vijijini lenye kata 21, lina jumla ya shule za sekondari za kata 25 na mbili za binafsi.

“Mbunge anahamasisha na kuchangia ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zote 27, lengo ni kuwapatia wanafunzi fursa nzuri ya kutoa elimu ya vitendo na kuongeza uelewa wao wa masomo ya sayansi,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa, ujenzi wa maabara hizo ni matayarisho ya jimbo hilo kuanzisha shule za kidato cha tano na sita.

“Tunakaribisha wengine wajitokeze kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye shule za Musoma Vijijini,” imesema taarifa hiyo.

1 Comment

  • @THINK/Dedication/Remember”@ EMPLOY/US THEM ALL – ALL TANZANIAN HAS JOB TO DO

    In 2021, the unemployment rate in Tanzania remained nearly unchanged at around 2.74 percent. With a decline of 0.04 percentage points, there is no significant change to 2020. Over the observed period, the unemployment rate has been subject to fluctuation.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari

Serikali yataka vijana  wajiunge na program atamizi ya biashara CBE

Spread the love  SERIKALI imewahamasisha vijana kujiunga na program atamizi inayotolewa na...

Elimu

Mfuko wa Jimbo Musoma Vijijini wamwaga mamilioni ujenzi maabara za sekondari

Spread the love  MFUKO wa Jimbo la Musoma Vijijini, Mkoa wa Mara,...

ElimuHabari

CBE yaanzisha Shahada 10 za Uzamili, CBE yajivunia wahitimu wanaoajirika

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimewataka wenye  kampuni na...

Elimu

Shule ya Alpha yazindua mfumo wa kugundua vipaji vya watoto

Spread the love  SHULE ya Sekondari ya Alpha ya jijini Dar es...

error: Content is protected !!