February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hans Poppe aachiwa kwa dhamana  

Spread the love

BAADA ya kufikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka mawili, hatimaye mwenyekiti wa kamati ya usajiri wa klabu ya Simba Zacharia Hans Poppe aachwa kwa dhamana yenye thamani ya shilingi 30 milioni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Kosa la kwanza alilosomewa Hans Poppe ni kutoa taarifa za uongo kwenye Mamlaka ya Mapato TRA kuhusiana na kiasi walichotumia kununulia nyasi bandia kwa ajiri ya ujenzi wa uwanja wa Simba uliopo Bunju.

Shitaka la pili linalo mkabili kiongozi huyo ni kungushi nyaraka za nyasi bandia ambazo hazina ukweli.

Ikumbukwe Hans Pope alitoa taarifa TRA kuwa Simba ilinunua nyasi kutoka nchini China kwa kiasi cha dola za kimarekani 45,577, sawa na pesa za kitanzania Sh. 105 milioni, kumbe uhalisia walinunua kwa Dola 109,499, sawa na Sh. 252 milioni.

Hans Poppe amedhaminiwa na watu wawili huku kila mmoja akiweka shilingi 15 milioni, na kesi hiyo imeahirishwa hadi tarehe 19 octoba, 2018.

error: Content is protected !!