August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hamissi arejeshwa MSCL baada ya kuondolewa TPA

Eric Hamissi

Spread the love

 

RAIS Samia Suluhu Hassan amemrejesha Eric Hamissi kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) baada ya kumwondoa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari hivi karibuni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hamissi alikuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa MSCL kabla ya Rais Samia kumteua kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TPA Aprili 4, 2021 cheo ambacho alikitumikia kwa mwaka mmoja na miezi mitatu kabla ya kuondolewa Julai 5, 2022.

Mkuu huo wa nchi amefanya uteuzi huo leo Alhamisi tarehe 4 Agosti, 2022, ambapo mbali na Hamissi pia amteua Stephen Kigaigai kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) akichukuwa nafasi ya Balozi Herbet Mrango ambaye amemaliza muda wake.

error: Content is protected !!