January 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hamisa Mabetto, Rick Ross wajiachia Dubai

Spread the love

 

MWANAMITINDO wa Tanzania, Hamisa Mobetto kwa mara ya kwanza amekutana na mwanamuziki wa Kimataifa kutoka Marekani, Rick Ross huko Dubai. Anaripoti Matilda Buguye, Dar es Salaam … (endelea).

Vipande vya video vimesambaa na kuteka mitandao mbalimbali ya kijamii kuanzia usiku wa kuamkia leo Ijumaa, tarehe 26 Novemba 2021, ikiwaonesha wawili hao wajiachia katika moja ya kumbi za Dubai.

Katika vipande hivyo vya video, Hamisa ambaye pia ni mfanyabiashara na Rick Ross wanajiachia mithili ya watu walioko kwenye mahusiano.

Hamisa amekutaka na msanii huyo maarufu duniani ikiwa imepita miezi takribani miezi sita, tangu alipofanya mahojiano na kuonesha kuvutiwa na msanii huyo wa Marekani kufanya nae kazi.

Mahojiano hayo yalifanyika Aprili 2021, kupitia Instagram (Instalive) na mkurugenzi wa kampuni ya kinywaji cha Belaire, Brett Berish kama muhamasishaji wa kinywaji hicho upande wa Afrika ya Mashariki.

Hamisa alipoulizwa anatamani kufanya kazi na msanii gani, alijibu kwamba, angetamani kufanya na Rick Ross.

Aidha, wakati huo urafiki wao umeendelea kushamiri hasa pale msanii huyo Rick Ross akionekana kuachia jumbe mbalimbali (coments) kwenye ukurasa wa instagram wa mrembo huyo bila kuchoka

error: Content is protected !!