May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Halmashauri zapewa angalizo

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania, amepiga marufuku vitendo vya ubaguzi vinavyofanyika katika utolewaji fedha za mikopo ya halmashauri nchini, kwa makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Anaripoti Nasra Bakari, DMC … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne, tarehe 8 Juni 2021, katika mkutano wake na wanawake wa Mkoa wa Dodoma, baada ya wanawake hao kulalamikia changamoto ya uhaba wa fedha hizo, zinazotolewa na halmashauri nchini.

Halmashauri zote nchini zimeagizwa kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani, kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi hayo, ambapo wanawake hupewa asilimia nne, vijana (4%) na watu wenye ulemavu (25) .

Rais Samia amemuagiza Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, Ummy Mwalimu, asimamie ugawaji wa mikopo hiyo, ili vikundi vyenye sifa vipewe fedha hizo.

“Kuhusu tuhuma za upendeleo katika kutoa mikopo ya halmashauri, namuagiza waziri wa Tamisemi usimamie, kwa vikundi vyenye sifa ya kupata, wapate isiwe kuvibagua,” amesema Rais Samia.

Wakati huo huo, amewaonya madiwani kutotumia mikopo hiyo kama fursa ya kujijenga kisiasa, kwa kuwa tabia hiyo inawalemaza wananchi kurejesha fedha wanaozaidiwa.

“Kwa kipindi kirefu madiwani mmekuwa mkitumia hii mifuko kujijenga kisiasa, ndiyo maana fedha hizo mzunguko wake unakuwa mdogo,”

“Mikopo hairudi sababu wanaoipokea wanahisi ni hisani kutoka kwa madiwani wao, hivyo mikopo hairudi. Niwaombe sana huu mfuko ni wamaendeleo kwa haya makundi,” amesema Rais Samia.

Aidha, Rais Samia ameziagiza halamshauri zitoe fedha nyingi kwa vikundi vichache, ili waweze kufanya biashara za uhakika, wapate fedha za kurejesha na kuongeza kasi ya mzunguko wake.

“Kiasi ambacho fedha kimekuwa kikitoka ni kidogo sana, kikundi cha watu sita kinapewa milioni moja wanafanya kitu gani?” amesema Rais Samia na kuongeza:

“ Ndiyo maana fedha hizio mzunguko wake ukawa mdogo, afadhali kutoa makundi machache yapate kiasi kikubwa, wasimamiwe wafanye la maana, warudishe mikopo wengine wapewe. Twende kwa mtindo huu,” amesema Rais Samia.

error: Content is protected !!