September 29, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Halmashauri zakumbushwa wajibu wake

Spread the love

SERIKALI imewataka viongozi wa halmashauri nchini kusimamia kikamilifu sheria ya usimazi wa mazingira ya mwaka 2004 katika maeneo yao,  anaandika Dany Tibason.

Na kwamba, hatua hiyo itasaidia kupunguza ongezeko la uharibifu wa mazinga unaofanywa nchini pia kukabiliana na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Hayo yamebainishwa leo Dodoma na Ngosi Mwihava, Naibu Katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais Mhandisi katika ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko tabia ya nchi.

Amesema kuwa, uharibifu wa mazingira unaofanywa katika maeneo mengi nchini unataokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu ambazo halmashauri zinatakiwa kuzikomesha kwa kusimamia sheria ya usimamzi wa mazingira ya mwaka 2004.

Mwihava amesema kuwa, sheria hiyo ya mazingira kama itasimamiwa kikamilifu uharibifu wa mazingiara utakomesha na Taifa litakuwa limeondokana na mabadiliko tabia ya nchi ambayo yamekuwa kero katika maeneo mengi Duniani.

“Uharifu unaofanywa wa mazingira unatokana na matumizi ya mkaa na kuni, kilimo pamoja na ufugaji wa kuhamahama ambavyo hivi vyote kama vitafanyiwa kazi katika maeneo husika suala la uharibifu wa mazingira halitakuwepo lakini pia tatizo la mabadiliko ya taibia ya nchi litapungua,”amesema Mwihava.

Amesema kuwa, halmashauri zinatakiwa kuhakikisha zipanda miti na si kuendelea kutegemea miti ya asili ili kuweza kudumisha uoto wa asili uliopo nchini.

Na kuwa, serikali imejipanga katika kuhakikisha inatafuta mbadala wa mkaa na kuni ambvyo ndivyo vimeonekana kuwa ni changamoto kubwa katika suala la uharibifu wa mazingira nchini.

“Kwa mjini tunapendekeza sana matumizi ya gesi ndomaana hata unaona kuwa tunapigania kushuka kwa bei ili kuweza kuondoa kabisa mazoea ya kutumia mkaa.

“…lakini kwa vijiji tunashauri watu watumie majiko banifu pamoja na bayo gesi inayotokana na kinyesi cha wanyama ili kupunguza matumizi ya mkaa na kuni,”amesema Mwihava.

Richard Muyingi, Kaimu Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais amesema, wameweka mkakati wa kuhakikisha kila halmasahari nchini inakuwa na wataalamu wa mazingira.

“Uwepo wa watu wa mazingira kama vile maofisa mazingira wa halmashauri kutasaidia kuhamasisha maendeleo ya mazingira katika halmashauri zao na kuondoa tatizo na uharibifu wa mazingira unaofanywa katika maeneo mbalimbali nchini,”amesema Muyungi.

Kharifa Msangi, mmoja wa washiriki katika warsha hiyo Ofisa wa Mazingira Mkoa wa Dodoma amesema, suala la upandaji miti ndiyo itakuwa mkombozi katika kukabilina na mabadiliko ya tabia ya nchi.

“Miti inaweza kuishi bila binadamu lakini binadamu hawezi kuishi bila miti hivyo kuna kila sababu ya kuhakikisha kuwa miti inapandwa kwa wingi ili kuweza kuendeleza uoto wa asili na watu kuendelea kupata hewa safi ya oxgeni inayotengenezwa na miti hiyo,”amesema Msangi.

error: Content is protected !!