January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Halmashauri zaagizwa kujenda nyumba za watumishi

Spread the love

SERIKALI imeziagiza halmashauri kutumia mapato yake ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo ilitolewa jana bungeni na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI, Selemani Jafo alipokuwa akijibu swalila mbunge wa Momba, David Silinde (Chadema).

Silinde pia aliuliza swali la nyongeza akitaka kujua ni kwanini mkoa mpya wa Songwe, haujapata mkuu wa mkoa wala mkuu wa wilaya pamoja na kukosekana kwa majengo wala ofisi.

Awali katika swali la msingi la mbunge huyo alitaka kujua ni kwanini serikali imekuwa ikisuasua kutoa fedha ili iweze kujenga ofisi na nyumba za watumishi katika makao makuu ya Wilaya ya Momba eneo la Chitete.

Jafo amesema katika mwaka wa fedha 2013/14 ilifanikiwa kupeleka fedha Sh. 250 milioni ambazo zimetumika kuanza ujenzi wa nyumba ya mkuu wa wilaya na nyumba mbili za viongozi waandamizi ambao umefikia hatua ya msingi.

“Katika mwaka wa fedha 2014/15 fedha zilizotengwa kwa kazi hizo hazikupelekwa aidha katika mwaka wa fedha 2015/16 serikali imetenga kiasi cha Sh. 287.7 milioni kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa nyumba hizo na Sh. 200 milioni zimetengwa kuanzia ujenzi wa ofisi ya mkuu wa wilaya,” amesema Jafo.

Amesema kwa upande wa ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Momba, serikali katika mwaka wa fedha 2014/15 ilitoa Sh. 450 milioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa ofisi hizo.

Amesema katika hatua ya kuhakikisha halmashauri inawapatia watumishi wake nyumba bora serikali imeziagiza halmashauri kutumia mapato ya ndani kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi.

Kuhusu kuwepo kwa mkoa wa Songwe Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais –TAMISEMI, George Simbachawene amesema mkoa huo bado haujatangazwa rasmi na pale utakapokuwa tayari utatangazwa katika gazeti la serikali na hatua wa ujenzi wa majengo utaanza.

error: Content is protected !!