June 19, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Halmashauri Dom zatoa msaada Kagera

Spread the love

JUMLA ya Sh. 46.3 milioni zimekabidhiwa kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutokana na michango ya halmashauri zote saba za Mkoa wa Dodoma pamoja na taasisi mbalimbali ili kusaidia wakazi  waliopata janga la tetemeko mkoani Kagera, anandika Dany Tibason.

Baada ya kupokea fedha hizo Waziri Mkuu ametangaza kuwa kila siku ya Jumanne atakuwa akikutana na wananchi pamoja na taasisi za watu binafsi ambao wapo tayari kutoa michango ya pole kwa wakazi wa Mkoa wa Dodoma waliopatwa na tetemeko la ardhi.

“Watanzania wenye nia ya kutoa msaada kwa waliokumbwa na maafa ya Kagera wawe na amani kwani serikali itahakikisha kuwa fedha zao na misaada vitatumika ipasavyo na itawatokea puani wale wanaodhani wataweza kujinufaisha kwa fedha hizo,” amesema.

Waziri Majaliwa alikuwa akizungumza na watumishi wa serikali pamoja na taasisi zake katika ukumbi wa mikutano wa CCM ambapo amewataka watumishi wa serikali waliopo katika mkoa wa Dodoma wawe tayari kuwapokea watumishi wageni.

error: Content is protected !!