December 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Halmashauri 164 kukusanya mapato kielektroniki

Spread the love

JUMLA ya halmashauri 164 sawa asilimia 90.6 nchini zimejiunga katika hatua mbalimbali za ufungaji na matumizi ya mfumo wa ukusanyaji wa mapato wa Kielektroniki. Anaandika Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na halmashauri hizo kujiunga katika mfumo bado halmashauri 17 mpya hazijajiunga katika mfumo huo wa ukusanyaji mapato.

Katika kuhakikisha mfumo huo unatumika ipasavyo wakuu wa mikoa yote wahakikishe majaribio ya matumizi ya mifumo iliyofungwa na inayoendelea kufungwa yanakamilika kabla ya Januari 31  mwaka huu ili kuongeza ukusanyaji wa mapato.

Hayo yalielezwa jana na Naibu Waziri,Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari juu utumiaji wa mfumo huo.

Amesema kuanzishwa kwa matumizi ya mfumo huo ni kuanzisha matumizi ya Benki na Tehama katika kukusanya kodi na tozo mbalimbali kwa lengo la kuongeza mapato.

“Hali hiyo inalenga kuondokana kabisa na utaratibu wa kukusanya mapato hayo kwa kutumia stakabadhi za kuandikwa kwa mkono ambayo utengeneza mianya ya wizi na ubadhirifu wa fedha.

“Kwa mamtiki hiyo,mfumo umekusudia kurahisisha utoaji wa stakabadhi na utunzaji wa kumbukumbu na kuthibiti upotevu wa mapato katika vyanzo vinavyokusanya fedha za Umma,” amesema Jafo.

Amesema mwanzo wa mfumo huo ni msingi wa matumizi ya kielektroniki ya malipo, kama Mpesa, Airtel Money, Point of Sale, Tigo pesa, Max Malipo na mifumo ya kibenki itakayowezesha walipa kodi kulipa kwa njia hiyo.

Amesema njia hiyo inatoa fursa ya uwazi ya uwazi katika makusanyo na kupunguza misongamano isiyo ya lazima.

Amesema ukusanyaji wa mapato kwenye serikali za mitaa inakusudia kuwepo kwa faida nne.

Amezitaja faida hizo kuwa ni kuongeza mapato kwa kasi zaidi kwa kuwa na uhakika wa makusanyo katika vyanzo vikuu.

Amesema kuweka uwazi na uwajibikaji katika makusanyo ya mapato,kupata vyanzo sahihi vya mapato na kufanya usulihishi kati ya kilichokusanywa na kilichotarajiwa kukusanywa.

Aidha alieleza kwamba kurahisisha uripaji miamala ya kodi na tozo itakayofanywa na walipa kodi.
Jafo amesema kitendo cha serikali kuweka mfumo huo kimefanikisha kuongeza makusanyo kati ya asilimia 800 na 900.

error: Content is protected !!