November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Halima Mdee: Nimeitwa polisi, sijui kuna nini?

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe

Spread the love

HALIMA Mdee, Mbunge wa Kawe na Mwenyekiti  wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA), amepokea wito wa Kamanda wa Upelelezi (RCO) Mkoa wa Kipolisi wa Kindoni, kwa ajili ya kufanyiwa mahojiano. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Taarifa ya wito huo imetolewa leo tarehe 23 Februari 2019 na Mdee kupitia ukurasa wake wa  mtandao wa kijamii wa Twitter.

Katika taarifa hiyo, Mdee ameandika kwamba ameitwa kwa ajili ya kuhojiwa katika Kituo cha Polisi cha Oesterbay, huku akieleza kuwa, hajui sababu ya wito huo.

“Nimepata WITO wa KUITWA POLISI OYSTERBAY kwa MAHOJIANO.Mpaka SASA sababu ya wito ni NINI. Ngoja TUJONGEE,” ameandika Mdee katika ukurasa wake wa Twitter.

error: Content is protected !!