August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Halima Mdee atupwa ‘jela,’ Mbowe asamehewa

Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (kushoto) akiwa mbele ya Kamati ya Haki na Maadili ya Bunge

Spread the love

KAMATI ya Haki na Maadili ya Bunge imetoa adhabu kwa Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kutohudhuria vikao vya Bunge la Bajeti vilivyobaki baada ya kumtia hatiani kwa kudharau mamlaka ya Spika na kutoa lugha ya matusi bungeni, anaandika Hamisi Mguta.

Uwamuzi huo umetekelezwa baada ya mjumbe wa kamati hiyo, Almasi Maige kuomba bunge lijadili na kutoa uamuzi.

Wakati huo huo, Kamati imetoa karipio kali kwa Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya, baada ya kukiri kosa la kudharau Bunge alilolifanya March 30, 2017.

Kamati hiyo pia imemsamehe, Freeman Mbowe kutokana na kosa la kutoa lugha isiyokuwa na staha kwa kuingilia Haki, Uhuru na Madaraka ya Bunge kwa sababu kosa lake lilikuwa la kwanza.

Mdee na Mbowe walikiri makosa kwenye kamati na kuomba radhi lakini kwakuwa Mdee ni kosa lake la pili kamati imechukua uwamuzi wa kumzuia kutohudhuria vikao hivyo vya Bunge la Bajeti.

error: Content is protected !!