August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Halima Mdee ashusha rungu kwa serikali ya JPM

Halima Mdee, Mbunge wa Jimbo la Kawe

Spread the love

HALIMA Mdee Mbunge wa Kawe amekosoa takwimu zinazotolewa na serikali kuhusu ukuaji wa uchumi pamoja na mikakati inayofanywa ili kunusuru anguko la uchumi, anaandika Faki Sosi.

Mdee amesema kuwa kitendo cha serikali kuondoa fedha kwenye benki za biasahara na kuzipeleka Benki Kuu nchi (B0T), kumeleta athari kubwa kwenye sekta ya kibenki inayochangia asilimia 30 ya pato la taifa.

Mdee amesema kuwa benki zimefunga milango ya kukopesha kutokana na uhakika wa kufanya biashara nchini kutokana na mzunguko wa fedha kuwa mgumu.

Wakati huo huo Mdee ameeleza kuwa Takwimu zilizotolewa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuwa pato limeongezeka ilhali Halmshauri zimenyang’anywa vyanzo vya mapato ambavyo TRA vimehodhi vyanzo hivyo na kujinadi kuwa wamefanikiwa kukusanya kodi nyingi bila kuonyesha mchanganuo wa mapato hayo.

TAZAMA VIDEO YOTE HAPO CHINI USISAHAU KU-SUBSCRIBE MwanaHALISI TV

error: Content is protected !!