April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Halima Mdee apeta Chadema

Spread the love

HALIMA James Mdee, ametetea kiti chake cha Uenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha) Taifa kwa kupata kura nyingi za ndio. Anaripoti Hamis Mguta … (endelea).

Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe, jijini Dar es Salaam ameshinda nafasi hiyo kwa kura 317 za ndio, ambazo saba zikimkataa na sita zikiharibika.

Katika kinyang’anyiro hicho, Mdee alipigiwa kura za ndio na hapana, kutokana na kuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo.

Mdee anaongoza baraza hilo kwa awamu ya pili, ambapo awamu ya kwanza ilikuwa 2014 alipopata kura 165, aliyemfuatia kwa karibu alikuwa Janeth Rithe aliyepata kura 35.

error: Content is protected !!