Thursday , 28 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Halima Mdee ambana Majaliwa bungeni kuhusu UVIKO-19
Habari za SiasaTangulizi

Halima Mdee ambana Majaliwa bungeni kuhusu UVIKO-19

Halima Mdee
Spread the love

 

MBUNGE viti maalum (asiye na chama bungeni), Halima Mdee, amehoji mikakati ya ziada ya Serikali katika kukabiliana na Ugonjwa wa Korona (UVIKO-19). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mdee amehoji swali hilo leo Alhamisi, tarehe 2 Septemba 2021, bungeni jijini Dodoma, katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

“Kwa kuzingatia changamoto ya Korona inapoteza watu wengi sana, hapa ukiuliza wabunge wangapi wamepoteza ndugu ni wengi. Nataka nijue Serikali ina mikakati gani ya ziada kukabiliana na hii changamoto, kwa mazingira ya ziada tofauti na mazingira yaliyopo sasa?” amesema Mdee.

Mbunge huyo wa viti maalum, amesema janga la Korona limepoteza maisha ya baadhi ya Watanzania, kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo ukosefu wa vifaa tiba vya kutibu ugonjwa huo na elimu ya kutosha juu ya kujikinga nalo.

Akijibu swali hilo, Waziri Mkuu Majaliwa amesema Serikali inashirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na nchi nyingine, kubaini namna ya kupunguza ama kutokomeza janga hilo.

“Tunashirikiana na WHO na kupata uzoefu wa wenzetu wanaokabiliana nalo, ili kuhakikisha kwamba tunapunguza ikiwezekana kuondoa kabisa maambukizi,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Majaliwa amesema, Serikali imekuwa ikihakikisha wagonjwa wa UVIKO-19, wanapata matibabu yanayostahiki hospitalini.

Aidha, Waziri Majaliwa amesema, Serikali inaendelea kushirikiana na wataalamu wa afya wa ndani, kutafuta tiba ya ugonjwa huo.

Majaliwa amewaomba Watanzania waendelee kufuata ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya, juu ya kujikinga maambukizi ya ugonjwa huo, ikiwemo kupata chanjo yake inayotolewa na Serikali nchi nzima.

“Tumeona kuna umuhimu wa kuchanja inasaidia kuweka virutubisho kwenye mwili, najua kuna vipingamizi watu wanapinga lakini kwa kutoelewa. Wale wanaopinga hawajaguswa na tatizo hilo ndani ya familia,” amesema Waziri Majaliwa.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Waziri Majaliwa amewatoa hofu Watanzania kuhusu uvumi unaotolewa na baadhi ya watu kwamba chanjo ya UVIKO-19 haifai, akisema haina madhara.

“Tumetumia wataalamu wetu wa ndani kufanya uchunguzi na wamefanya hivyo, tumewatumia madaktari ambao ni ndugu zetu wamebobea kwenye sekta ya afya na wanaamika nje,” amesema Waziri Majaliwa na kuongeza:

“Tumejiridhisha, sababu hatuamini daktari huyu Mtanzania, ana ndugu akashauri achanje chanjo ambayo itakuja kumpotezea maisha yake.”

Mdee ameendelea kuulizwa swali eneo hilo katika kipindi cha maswali na majibu, akiuliza swali la nyongeza akisema “watu wengi wanakufa kwa kukosa mitungi ya gesi. Nini mkakati wa serikali ili kuhakikisha wananchi wanapata mitungi ya gesi na wasife kwa kukosa oksijeni.”

Akijibu swahi liho, Naibu Waziri wa Tamisemi, Dk. Festo Dugange amesema, “kumekuwa na upungufu wa baadhi ya vifaa tiba katika hospitali zetu na serikali imekuwa inaongeza vifaa na vitendanishi.”

Amesema, bado kuna changamoto kwa vifaa tiba hususan mitungi ya gesi na serikali inalifanyia kazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

Habari za SiasaTangulizi

Vikundi hewa 851 vyalamba bilioni 2.6 mikopo ya halmashauri

Spread the loveVIKUNDI hewa vya wajasirimali wadogo 851 kutoka katika halmashauri 19...

Habari za SiasaTangulizi

Mashirika matano yapata hasara mabilioni ya fedha

Spread the loveMASHIRIKA matano ya Serikali yanayojiendesha kibiashara, yamepata hasara ya mabilioni...

error: Content is protected !!