Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Hali ya kisiasa Tanzania yampeleka Mbowe Marekani
Habari za Siasa

Hali ya kisiasa Tanzania yampeleka Mbowe Marekani

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

MWENYEKITI wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe, anatarajia kufanya ziara ya kikazi ya siku sita nchini Marekani, ambapo atafanya mazungumzo na viongozi wa kimataifa kuhusu hali ya kisiasa Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Taarifa ya ziara hiyo imetolewa leo Jumapili, tarehe 4 Desemba 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itifaki na Mambo ya Nje Chadema, John Mrema.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mrema, Mbowe anatarajiwa kuondoka nchini leo kuelekea Marekani.

Taarifa ya Mrema imesema kuwa, Mbowe atahudhuria Kongamano la Umoja unaoshughulika na masuala ya demokrasia (International Democrat Union -IDU), litakalofanyika siku tatu na kuhudhuriwa na viongozi na wanachama wanaotokana na vyama vya siasa wanachama wa umoja huo.

Pia, Mbowe atahudhuria kongamano la Baraza la Uongozi la IDU kama mwenyekiti mwenza wa Democrat Union of Africa (DUA).

“Akiwa Marekani Mbowe atafanya mfululizo wa vikao na viongozi mbalimbali duniani pamoja na taasisi na mashirika ya kimataifa kuhusiana na haki ya kisiasa nchini Tanzania Kwa nafasi yake kama mwenyekiti wa Chadema. Kadhalika, atakutana na mashirija na viongozi mbalimbali kujadikiana Hali ya demokrasia, utawala wa Sheria na maendeleo ya kiuchumi barani Afrika kama Mwenyekiti mwenza wa DUA,” imesema taarifa ya Mrema na kuongeza:

“Mbowe anatarajiwa kuhitimisha ziara yake Kwa kuzungumza na Watanzania waishio Marekani tarege 10 Desemba 2022 jijini Washington.”

2 Comments

  • PROFESSA ASSAD ALITUFAHAMISHA UBADIRIFU WA TAASISI ZETU BILA KUMUN’GUNYA. BADALA YA KUMSHUKURU AKAONDOLEWA KINYUME NA KATIBA. UKWELI WAKO HAUKUWA NA KASORO YOYOTE LAKINI HAUKUPENDWA. WALIOTAKIWA KUULEWA UKWELI WAKO HAWAKUUPENDA. KWA AJABU LEO NINASOMA MHESHIMIWA WAZIRI MKUU AKILAUMU WAKAGUZI HESABU WAZEMBE. NASHINDWA KUWAELEWA VIONGOZI WETU. PROF ASSAD HAKI IMEDHIHIRISHA HAKI YAKO. WASTAHILI KULIPWA MASLAHI YAKO KWA MUDA WAKO WOTE WA KAZI KIKATIBA. UKWELI WAKO WAKO NA UJASIRI WAKO KAMWE HAUTASAHURIKA!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!