Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Hali ya dawa za kulevya Tanzania, bangi….
Habari Mchanganyiko

Hali ya dawa za kulevya Tanzania, bangi….

Spread the love

 

KATIKA mwaka 2021 tani 22.74 za bangi zilikamatwa ikiwa ni ongezeko la asilimia 72 ya kiasi kilichokamatwa mwaka 2020. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa, tarehe 10 Juni 2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu-Sera, Bunge na Uratibu, George Simbachawene alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2021.

Amesema ukamataji huo ulihusisha jumla ya watuhumiwa 9,484 wakati huo mirungi iliyokamatwa katika kipindi hicho ilifikia tani 10.93 zikihusisha watuhumiwa 1,395.

Aidha, Simbachawene amesema kwa upande wa dawa za kulevya zinazozalishwa viwandani, mwaka 2021 jumla ya tani 1.13 za heroin zilikamatwa.

“Hiki ni kiwango kikubwa kuwahi kukamatwa mwaka mmoja katika historia ya nchi yetu. Kiasi hicho ni mara tatu ya kiasi kilichokamatwa mwaka 2020, aidha katika kipindi hicho kiasi cha gramu 811.30 za Cocain zilikamatwa” amesema Simbachawene.

George Simbachawene, Waziri wa Mambo ya Ndani

Aidha amesema kwa mara ya kwanza mwaka 2022 katika historia ya mapambano dhidi ya dawa za kulevya nchini shehena kubwa ya jumla ya kilo 430.77 za dawa za kulevya aina ya methamphetamine inayotengenezwa na kemikali bashirifu ilikamatwa, ikihusisha watuhumiwa tisa raia wa Iran wote wakiwa wanaume.

“Katika kukabiliana na tatizo hilo, Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa uingizwaji na matumizi ya methamphetamine pamoja na kemikali bashirifu ambazo hutumika kutengeneza dawa hizo.

“Tatizo la matumizi ya dawa za kulevya nchini limeendelea kuwepo pamoja na juhudi za udhibiti zinazofanywa na serikali. Hadi kufikia mwezi Desemba 2021, waraibu wa dawa mbalimbali za kulevya pamoja na vilevi vingine wapatao 905,902 walijitokeza kupata tiba katika hospitali za wilaya na mikoa nchini.

“Serikali imeendelea kupanua wigo wa matibabu kwa waraibu wa dawa za kulevya ambapo hadi kufikia mwezi Desemba, 2021 huduma za tiba ya uraibu zilikuwa zikipatikana kwenye vituo 15 vya kutolea tiba kwa waraibu wa heroini (MAT Clinics) na vituo hivi kwa pamoja vilikuwa vimesajiri waraibu 11,650.

Baadhi ya dawa za kulevya

“Vituo hivi vinapatikana katika mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Tanga, Mbeya, Songwe, Dodoma, Mwanza na Arusha. Serikali imeendelea kufanya usimamizi katika nyumba 44 za Upataji Nafuu (Sober House) nchini.”

Waziri Simbachawene amesema,”nyumba hizi huanzishwa na kuendeshwa na asasi za kiraia na Serikali kwa kupitia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imetengeneza Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Nyumba za Upataji nafuu nchini.”

“Mwongozo huu unasaidia kuzifanya nyumba hizi kutoa huduma za utengamao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizopo”. amesema Simbachawene.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Gardner Habash wa Clouds Fm afariki dunia

Spread the loveALIYEKUWA mtangazaji wa kipindi cha Jahazi kinachorushwa na kituo cha...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

error: Content is protected !!