Thursday , 25 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Hali mbaya Somalia
Habari Mchanganyiko

Hali mbaya Somalia

Spread the love

HALI mbaya ya hewa, wimbi la mkaundi ya nzige yaliyovamia nchi hiyo pamoja na mvua za kiwango cha chini, zimelifanya Taifa la Somali kuzama kwenye waziwasi wa maafa ya njaa. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Tayari Shirika la kimataifa la Misaada ya Kibinaadamu – Save the Children – limeeleza, mazao nchi humo yanatarajiwa kupungua kwa asilimia 80 na kuifanya nchi hiyo kuingia kwenye hatari kubwa ya njaa.

Kutokana na hali hiyo, mapato yanayotokana na mauazo ya mifugo, ambayo ndio uti wa mgongo wa uchumi wa Somalia, yanatarajiwa kushuka hadi asilimia 55.
Shirika hilo limeeleza, mlo mmoja kwa sasa umekuwa tabu zaidi nchini humo, na kwamba wanawake wamekuwa nguzo kubwa ya kusaka chakula cha siku nchini humo.

Utafti wa shirika hilo umeeleza, kwa mwaka huu ni asilimia 15 tu ya chakula inayoweza kufikiwa na familia masikini nchini Somalia, baadhi ya watoto tayari wana utapiamlo.

Wasomali tayari wanakabiliwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na ghasia za muda mrefu za wanamgambo wa kiislamu, hali tete ya kisiasa na miaka 30 ya kutokuwa na Serikali Kuu yenye ufanisi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!