May 25, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hali ilivyo St. Peter kwenye Ibada ya Dk. Magufuli

Mwili wa aliyekuwa Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli ukitoka Ikulu jijini Dar es Salaam

Spread the love

 

VIKOSI vya usalama vimeimarisha ulinzi kila mahali, waombolezaji na watu mbalimbali wanaingia kwa kutumia mlango mmoja. Anaripoti Mwandishi Wetu

Kila anayeingia eneo hili analaguliwa lakni pia anapewa kitakasa mikono(sanitizer), sehemu za kuegesha magari eneo lianalozunguka kanusa limejaa.

Vikosi vya usalama vinaelekeza wenye nagari kwenda mele zaidi kutafuta eneo LA kuegesha magari, barabara ya Ali Hassan Mwingi ni nyeupe kwa maana askari wa usalama barabarani wamesimama kila njia panda ya kuingia barabara hiyo.

Uwanja wa kanisa vikosi vya Jeshi la Wananchi (JWTZ), vimechukua sehemu kubwa ya ulinzi, utulivu unetawala eneo hili huku nyimbo za maombolezo zikiendelea kuimbwa.

Mwili huh umeingia kanisani hapo ukitokea Ikulu ya Magogoni jijini Dar es Salaam ente alilohudumu kwa takribani Milka mitant na meiji mitano.

Watumishi wa Ikulu, walipata fursa ya kumuaga kwa kumpungia mkono jeneza lililokuwa limebeba mwili wa Dk. Magufuli ambaye atazikwa Ijumaa tarehe 26 Machi 2021, nyumbani kwao Chato mkoani Geita.

error: Content is protected !!