August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Hakuto tayari kudhalilika’

Spread the love

HATUKO tayari kudhalilika kwa kupokea fedha za wafadhili ambazo mashariti yake yanakiuka utu, mila na utamaduni wa kitanzania, anaandika Dany Tibason.

Hivyo halmashauri zote nchini, zikusanya mapato pia zitumie fedha hizo kwa matumizi sahihi na yanayoelezeka.

Hayo yameelezwa na Samia Suluhu Hasani, Makamu wa Rais alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya wakazi wa Dodoma muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake ya ukaguzi wa dampo la kisasa, pamoja na ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambayo kwa sasa imekabidhiwa Ikulu ili ilipangie matumizi.

Samia amesema halmashauri nyingi zimekuwa zikilalamika kuwa, hazina mapato wakati wamekuwa wakikusanya fedha nyingi na kuzitafuna badala ya kuzielekeza katika shughuli za maendeleo.

Amesema, kitendo cha halmashauri kutokusanya mapato na kuipatia serikali fedha za kutosha, kumepelekea wafadhili kuilazimisha serikali kuwapa fedha kwa mashari ambayo hayawezi kukubalika kwa desturi za kitanzania.

“Wafadhili wamekuwa wakilazimisha kutoa misaada kwa masharti magumu ambayo yanadhalilisha utu, mila na tamaduni na pale mnapowakatalia, wanaondoa fedha hizo na wanaangalia sehemu nyeti zaidi.

“Mfano wakiona mmewakatalia kupokea misaada kwa masharti wanayoyataka, wanaondoa fedha kama vile dawa za kurefusha maisha (ARVs) wakijua watu wakikosa hizo dawa watakufa,” amesema.

Amesema kutokana na serikali kutopenda kutegemea zaidi fedha za misaada, inazitaka halmashauri zote kuhakikisha zinakusanya mapato kwa kutumia mashine za kielektoniki na fedha hizo ziweze kutumiwa vyema kwa matumizi sahihi.

Katika hatua nyingine amesema, ili Dodoma iwe Jiji ni lazima viongozi wa mkoa washirikiane vyema na halmashauri kwa kuangalia ni jinsi gani ya kuweza kukidhi vigezo.

Mbali na hilo Samia ameitaka Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu (CDA) kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wafanye kazi ya uboreshaji mji pamoja na upimaji wa viwanja kama inavyotakiwa.

Amesema, CDA ni ya muda mrefu lakini imekuwa haifanyi kazi kwa kiwango kinachoridhisha jambo ambalo linaonekana kudhoofisha kasi ya ukuaji wa mji wa Dodoma.

error: Content is protected !!