August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hakimu Kisutu ‘awawakiwa’ Mdee, Mwita

Spread the love

HATUA Halima Mdee, Mwita Waitara kutofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam kuendelea na shauri la kesi yao, imemkera hakimu Huruma Shahidi, anaandika Faki Sosi.

Ni katika kesi ya kumjeruhi Terresia Mbando, Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam wakati wa hekaheka za uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam.

Kwenye kesi hiyo pia yumo Saed Kubene, Mbunge wa Ubungo ambapo Mdee ni Mbunge Kawe na Waitara ni Mbunge wa Ukonga.

Mdee na Waitara hawakufika mahakamani hapo leo ambapo Frederick Kiwelo, wakili wa upande wa walalamikiwa ameimbia mahakama kuwa, mteja wake Mdee yupo nje ya nchi (Canada) na Waitara anamuuguza mtoto wake Tarime mkoani Mara na pi naye ni mgonjwa.

Hata hivyo, hakimu Shahidi hakuridhishwa na utetezi huo ambapo amesema kuwa, washitakiwa Mdee na Waitara hawakuwa na sababu za msingi za kutohudhulia mahakamani.

Amesema kwamba, Mdee amekwenda nje ya nchi kwa sababu zake binafsi huku akijua siku ya kesi yake hivyo amewataka kuheshimu taratibu za sheria.

Watuhumiwa mwengine katika kesi hiyo ni Efraim Kinyafu, aliyekuwa Diwani wa Saranga, na Shafii Juma.

Leo washitakiwa wawili wapya wameunganishwa kwenye keshi hiyo ambao ni Edwin Mwakato, Diwani wa Liwati na Edwan Mwaipaja, Diwani wa Segerea.

Awali Anastazia Wilson, wakili wa serikali mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, amewasomea mashitka washitakiwa hao wawili na kuunganishwa pamoja na washitakiwa wengine kwa shitaka la kumjeruhi Mbando.

Kesi hiyo itatajwa tena tarehe 28 Agosti kwa ajili ya kusemowewa maeleza ya awali.

error: Content is protected !!