HEREN Liwa, Hakimu Mkazi katika Mahakama ya Kisutu, Dar es Salaam amelalamikia tabia ya mawakili/waendesha mashitaka kushindwa kukamilisha ushahidi hivyo kusababisha kesi kuchelewa, anaandika Happyness Lidwino.
Hakimu Liwa amewataka waendesha kesi na mawakili wa serikali kukamilisha uchunguzi wa mashitaka ili kutoa hukumu ya kesi mapema ili kuepuka malalamiko kutokwa kwa wananchi.
Amesema hao wakati akisikiliza kesi mbalimbali katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo kesi tano alizokutana nazo leo, uchuzi nguzi wake ulikuwa haujakamilika.
Amesema kuwa, licha ya kuwa ni amri kutoka ngazi za juu lakini yeye pia hapenzi kuona watu wakiteseka rumande.
More Stories
Exim waadhimisha miaka 25, yapongeza wafanyakazi wake
NMB yamwaga vitanda, magodoro Kagera
NBC wasisitiza kukuza michezo, sanaa na utamaduni