May 15, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Hakimu amvutia pumzi Lissu

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara

Spread the love

TUNDU Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), amekwama kuhudhuria kesi yake ya uchochezi namba 236/2017 na 123/2017 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Imeelezwa, Lissu ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Bara ameshindwa kuhudhuria kesi hiyo kutokana na kuchelewa kutoka Makao Makuu ya Tume ya Uchaguzi (NEC), Dodoma baada ya kurejesha fomu zake za kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Leo Jumatano tarehe 26 Agosti 2020, Wakili wa Serikali Mkuu, Simon Wankyo akisaidiwa Renatus Mkude mbele ya Hakimu Mkazi, Augustina Mbando wameeleza, wakili wake (Lissu) aliahidi kwamba mtuhumiwa huyo angekuwepo leo mahakamani hapo.

Ni baada ya awali, wakili wa Lissu, Peter Kibatala kuieleza mahakama kwamba, mteja wake (Lissu) amerejea nchi kutoka kwenye matibabu na alijiweka karantine kwa siku 14.

Taarifa ya Lissu kushindwa kuhudhuria kesi yake ya uchochezi, imetolewa na mdhamini wake Rose Moshi, akieleza “mchakato huo (urejeshahi fomu) uliisha jana saa mbili usiku.”

Mahakamani hapo, kauli ya mdamini wa Lissu haikupata pingamizi lolote kutoka upande wa Jamhuri, hivyo Hakimu Mbando ameahirisha shauri hilo mpaka tarehe 24 Septemba 2020.

Kwenye shauri hilo, Lissu anatuhumiwa kwa kutoa maneno ya uchochezi. Inadaiwa tarehe 17 Julai 2017, Kinondoni jijini Dar es Salaam, alitoa maneno ya kujaza chuki.

Tundu Lissu, Mgombea Urais wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, akirudisha fomu ya kuteuliwa nafasi hiyo kwa Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage

Katika shauri namba 123 la mwaka 2017, lililotajwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Kassian Matembele leo, Wakali Kibatala ameeleza mahakama hapo kuwa, Lissu ameshindwa kuhudhuria kwa sababu ya kuchelewa kukamilisha taratibu za urejeshaji wa fomu ya NEC.

Shauri hilo nalo limeahirishwa hadi tarehe 24 Septemba 2020. Kwenye shauri hilo, Lissu anakabiliwa na tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi.

Inadaiwa kuwa, tarehe 11 Januari akiwa  Kombeni mkoani Mjini Magharibi Zanzibar kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Diman, anadaiwa kutoa maneno yenye udini na yenye kuchochea.

error: Content is protected !!