October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hakimu agoma kumpa dhamana mtuhumiwa sugu wa bangi

Spread the love

MOHAMED Hamis, mtuhumiwa aliyekutwa na bangi yenye uzito wa kilo 0.57 amekataliwa dhamana kutokana na kuwa ‘mzoefu’ kukamwata na makossa ya namna hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika Mahakama ya Mkazi Kinondoni jijini Dar es Salaam, Hakimu Bonifasi Lihamwike ameeleza kuwa, hatompa dhamana Mohamed (24) kwa kuwa, tayari amefikishwa kwenye mahakama hiyo mara nne kwa kosa moja.

Akisomewa shitaka hilo mbele ya Hakimu Bonifasi Lihamwike, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Veronika Mtafia alidai kuwa Januari 10, mwaka huu eneo la Sinza Kwa Mori, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam mshitakiwa alikutwa na kiasi hicho cha dawa za kulevya huku akijua ni kinyume cha sheria.

Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo huku upande wa Jamhuri ukisema upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kuomba tarehe ya kutajwa tena.

Hata hivyo, Hakimu Lihamwike amesema, kutokana na mtuhumiwa kurudishwa mara nne mahakamani kwa wakati tofauti kwa tuhuma ya kukutwa na dawa za kulevya, mahakama imeamua kutompa dhamana kwa kesi hiyo mpaka hukumu itakapotolewa.

Hemed amerudishwa rumande hadi kesi yake itakaposomwa tena tarehe 25 Machi 2019.

error: Content is protected !!