Thursday , 18 April 2024
Home Kitengo Maisha Elimu HakiElimu yaeleza changamoto mtoto wa kike
Elimu

HakiElimu yaeleza changamoto mtoto wa kike

Wanafunzi wakiwa darasani
Spread the love

KUTEMBEA mwendo mrefu pia kushindwa kupatikana kwa mahitaji kwa mtoto wa kike, husababisha watoto hao kufikiria kuacha shule. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hiyo ni sehemu ya utafiti uliofanywa na Shirika lisilokuwa la kiserikali nchini HakiElimu, kuhusu ElimuMsingi kwa wasichana Tanzania.

Akiwasilisha utafiti huo Dk. John Kalage, Mkurugenzi Mtendaji HakiElimu mbele za wadau na mgeni rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia, Dk. Leonard Akwilapo jijini Dodoma amesema, utafiti huo umehusisha mikoa mitano.

Amesema, mwaka huu HakiElimu imefanya utafiti kujua sababu za mtoto wa kike kushindwa kubakia shule na kujifunza ipasavyo pamoja na kufaulu kutoka ngazi moja ya elimu kwenda nyingine.

Na kwamba, utafiti huo kwa ujumla umegundua sababu za msingi zinazochangia kuwazuia wanafunzi wa kike kubaki shuleni, na kumaliza elimu ya msingi na kwenda elimu ya sekondari.

“Kwa ufafanuzi, tunaposema kubaki shuleni kwa wanafunzi wa kike inamaanisha kubaki kusoma shuleni mpaka kumaliza ngazi ya elimu husika au kupata ujuzi na maarifa husika kutoka ngazi moja ya elimu kwenda ngazi nyingine,” ameeleza Dk. Kalage.

Amesema, utafiti uliofanywa na HakiElimu, umefanyika katika mikoa mitano ambayo ni Dar es Salaam, Lindi, Kilimanjaro, Dodoma na Tabora na wilaya 12, kaya 24 na shule 63 zilichaguliwa kushiriki katika utafiti huo.

https://www.youtube.com/watch?v=f9CG9ymEpX8

Hata hivyo Dk. Kalage amesema, wakati utafiti unafanyika, asilimia 10.8 ya wasichana waliosailiwa waliripoti kuwa wamewahi kufikiria kuacha shule kwasababu ya ukosefu wa mahitaji muhimu ya shule na maisha kwa ujumla, ili waweze kujitafutia mahitaji yao au kusaidia juhudi za wazazi au walezi katika kutafuta mahitaji.

Katika changamoto ambazo zinawakumba watoto wa kike kuendelea na masomo ni pamoja na kutebea mwenendo mrefu, kukosekana kwa mahitaji muhimu, jambo ambalo linasababisha kujiandikisha kwa wingi shuleni lakini wanaomaliza ni wachache.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu Sayansi na Teknologia Dk. Leonard Akwilapo amesema, wanakubaliana na utafiti wa HakiElimu na utafiti huo unaifanya serikali kupambana na changamoto zinazomkabili mtoto wa kike.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanawake GGML wawanoa wanafunzi Kalangalala Sec. kujitambua

Spread the loveKATIKA kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Umoja wa...

error: Content is protected !!