July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Haji Manara atangaza kung’atuka Simba

Haji Manara

Spread the love

 

HAJI Manara, Msemaji wa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21, Simba ya Dar es Salaam, ametangaza kung’atuka katika nafasi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Manara ametangaza uamuzi huo leo Jumatano, tarehe 21 Julai 2021, ikiwa ni siku takribani tatu zimebaki kabla ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho kati ya Simba na Yanga.

Watani hao za jadi, wanakutana katika fainali hiyo, Jumapili tarehe 25 Julai 2021, katika Uwanja wa Tanganyika, mkoani Kigoma.

Simba inakwenda katika fainali hizo, ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha 1-0 ilichokipata tarehe 3 Julai 2021, kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa ligi kuu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Haji Manara, Afisa Habari wa Simba

Aidha, Simba inashuka kwenye fainali hizo kutetea ubigwa wa michuano hiyo na ikiwa tayari imetetea mara ya nne mfululizo ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Manara ambaye ni mmoja wa wasemaji machachari zaidi Tanzania kwa ngazi ya klabu, ameandika maelezo ya kutaka kukaa kando kwenye nafasi hiyo.

Manara ameandika hivi;

Kila la kheri jumamosi Inshaallah na Mungu awabariki wote.

Bad luck Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu sitakuwepo kigoma na pia naomba nipumzike kdogo ktk magroup ya mpira ili nipate muda wa kutafakari kdogo,,,,,,

Nimeonewa vya kutosha na imefika muda wa kutafakari juu ya mustakabali wa maisha yangu yajayo,,,

Nisameheni wote niliowakwaza katika utumishi wangu Simba na lolote nililofanya Kwa makosa basi ni ktk kutimiza majukumu yangu klabuni,,,,

Kwa kiapo changu sitatoa sababu ya uamuzi huu Kwa maslahi mapana ya klabu hii ninayoipenda mno,,,,

Kama uhai utakuwepo basi Inshaallah msimu ujao sitakuwa nanyi Msimbazi,,,

Again isije kuwa nimemkwaza mtu mkanilaumu Naomba sana radhi na mengine namuachia Mungu tu.

error: Content is protected !!