September 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Haiti yakubwa na tetemeko kubwa, laua 304 na 18,000 wajeruhiwa

Spread the love

 

TETEMEKO la ardhi lenye ukumbwa wa vipimo vya Ritcher 7.2 limeikumba nchi ya Haiti na kusababisha vifo vya takribani watu 304, kujeruhi 1,800 pamoja na kuharibu nyumba na miundombinu mbalimbali. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Miongoni mwa uharibifu umejitokeza kutokana na tetemeko hilo lililotokea jana Jumamosi tarehe 14 Agosti 2021, ni majengo makubwa, hoteli, nyumba za makazi, makanisa huku Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Ariel Henry akitangaza mwezi mmoja wa hatari akisema kilichotokea ni uharibifu mkubwa.

Waiziri Mkuu huyo amesema, tayari amekwisha kuandaa timu ya kutoa msaada kwa wahanga wa tetemeko hilo akisisitiza “kitu cha muhimu ni kuokoa manusura wengi iwezekanavyo waliokwama kwenye vifusi.”

Amesema, hospitali mbalimbali zimeelemewa na majeruhi hususan Hospitali ya Les Cayes inayowahudumia wale waliojeruhiwa na waliovunjika.

Kutokana na kadhia hiyo, Rais wa Marekani, Joe Biden amesema, Taifa lake, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) litasaidia kutathimini uharibifu na kuwaokoa wale waliojeruhiwa na wale ambao watalazimika kujenga tena.

“Katika kile ambacho ni wakati mgumu kwa watu wa Haiti, Nimefadhaishwa na tetemeko hili,” alisema Rais Biden.

Waandishi wa habari waliokuwa Le Nouvelliste walisema makanisa mengi na hoteli katika pwani ya kusini zimeporomoka au kuharibiwa vibaya.

Archdeacon Abiade Lozama, mkuu wa kanisa la Episcopal mjini Les Cayes, aliiambia gazeti la New York Times, “barabara zilijaa kelele. Watu walikuwa wakiwatafuta wapendwa wao, mali zao au huduma ya afya na maji.”

Leila Bourahla, Mkurugezi wa shirika la Haiti la Save the Children, ameliambia gazeti la New York Times kwamba itachukua siku kadhaa kutathmini uharibifu lakini “ni wazi kuwa hili ni janga kubwa la kibinadamu”

Naomi Verneus, 34- mkazi wa jiji kuu la Port-au-Prince, aliliambia shirika la habari la Associated Press kwamba aliamshwa na mtetemeko huo na kitanda chake kilikuwa kikitikisika.

“Nilipoamka sikuwa hata na muda wa kuvaa viatu. Tuliponea tetemeko la ardhi la mwaka 2010 kwa hivyo kilichonijia akilini ni kukimbia. Baadae nilikumbuka watoto wangu wawili na mama yangu mzazi walikuwa ndani ya nyumba. Majirani zangu walienda kuwaambia watoke nje. Tulikimbia barabarani,” alisema.

Mwaka 2010 tetemeko la ardhi lilokumba Haiti liliwaua watu zaidi ya 200,000 na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na uchumi.

error: Content is protected !!