KIUNGO wa zamani wa klabu ya Manchester United na timu ya taifa ya Uingereza, Owen Hagreves amesema Maichael Carrick ndio mchezaji sahihi wa kucheza na Paul Pogba katika eneo la kiungo kutokana na aina ya uchezaji wake aliouonesha jana dhidi ya Fenerbahce walioibuka na ushindi wa mabao 4-1.
“Aina ya uchezaji wa Carrick hauna tofauti sana na Pirlo ambaye alifanya Pogba kuwa katika kiwango bora alipokuwa Juventus walipokuwa wakicheza wote katika eneo la kiungo,” amesema Hagreves.
Mchezo wa jana ndiyo ulikuwa wa kwanza kwa Pogba na Carrick kucheza pamoja na kuonekana kucheza vizuri nakufanikiwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao manne waliyoyapata jana na kuonesha mchezo mzuri uliowapa matumaini mashabiki wa Manchester United.
Hagreves aliongezea kuwa, anajua Mourinho anajaribu kutafuta mtu sahihi wa kucheza na Pogba katika timu hiyo lakini anaweza kumtumia Carrick katika timu hiyo kutokana na kiungo huyo kuwa na ufanisi katika eneo la katikati ya uwanja.
Pogba ambaye kwa sasa ndiye mchezaji ghali ulimwenguni, amekuwa katika wakati mgumu kutokana na kutoonyesha ubora wake toka aliporejea kwenye klabu baada ya miaka minne, kitu kinachopelekea kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho kujaribu na wachezaji tofauti tofauti ili aweze kupata mfumo utakaomfanya kiungo huyo kucheza vizuri.
More Stories
Yanga yaanza safari ya kutetea ubingwa wake
Ngao ya Jamii kuchezwa kwa mtoano
KMC yatua Arusha kibabe