June 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Hafla ya wasanii kumuaga Rais Kikwete utata mtupu

Rais Jakaya Kikwete (wa pili kushoto) akiwa katika hafla ya kuagwa na wasanii. Kushoto ni Katibu wa CCM, Abdulahaman Kinana. Kutoka kulia ni Waziri wa Sayansi na Tekinolojia, Januari Makamba na Mgombea wa CCM, John Magufuli.

Spread the love

HAFLA inayotajwa kuandaliwa na “Umoja wa Wasanii Tanzania” ya kumuaga Rais Jakaya Kikwete anayestaafu baada ya uchaguzi wa Okotoba mwaka huu, imezua mjadala mkubwa nchini. Anaandika Erasto Stanslaus … (endelea).

Mjadala wenyewe unatokana na kile ambacho wengi wa wasanii wanasema kwamba hawajapata kujua kwamba kuna umoja wa wasanii Tanzania.

Mingi ya mijadala inayoendelea kwenye kota mbalimbali za jiiji la Dar es Salaam pamoja na mitandao ya kijamii yanajadili kwamba kama ni umoja wa wasanii kumuaga Rais kikwete, imekuaje ukumbi umejaa makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwepo mgombea Urais wa chama hicho katika uchaguzi mkuu huo, John Magufuli.

Hoja kuu hapa ni, Je, umoja huo wa wasanii umeundwa ndani ya mfumo wa CCM? au wasanii waliokuwa mbele katika hafla hiyo walitumika tu kujenga picha kwamba umma wa wasanii Tanzania unamsapoti Magufuli?

Ukweli ni kwamba, katika miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa katika tasnia ya filamu na muziki, ukiwemo wa bongo fleva, taarabu, muziki wa injili na dansi, wapo wengi siyo tu ni viongozi katika vyama vya upinzani, pia ni wagombea nafasi za ubunge kupitia vyama hivyo vya upinzani.

Baadhi wa wasanii ambao ni wagombea ni Seleman Msindi ‘Afande Sele’ na Joseph Haule ‘Prof. Jay’. Wasanii waliokuwa meza kuu katika hafla hiyo sambamba na Kikwete ni Jacob Steven ‘JB’ na Nikii wa Pili.

Yafuatavyo ni maswali yanayouliwa katika mijadala iliyopo katika mitandao ya kijamii:-

  1. Umoja huo umeanzishwa lini na viongozi wao kina nani?
  2. Wasanii wanatambua kua kuna umoja wa wasanii tena usiokua na jina rasmi?
  3. Kama wasanii wameungana ili kumuaga rais wa nchi, kwanini kulikuwa na lundo la viongozi wa chama kimoja cha siasa?
  4. Magufuli kupewa nafasi ya kipekee, alienda kama mgombea wa chama, kama waziri au kama mpiga ngoma mtarajiwa wa Twanga?
  5. Nani aligharamia gharama za sherehe?
  6. Wasanii walizipataje hizo pesa za sherehe wakati wenzao wakiumwa hadi waandae matamasha ya kuchangia kwa njia ya kiingilio na hawapati zaidi ya Sh. milioni mbili.
  7. Kwanini wasanii ambao ndio wanaodaiwa kuwa waandaaji waliandaliwa kadi za mwaliko badala ya wao kumuandalia mheshimiwa rais kadi ya mwaliko?
error: Content is protected !!