January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gwaride, ngoma za asili zapamba sherehe za Mapinduzi Zanzibar

Spread the love

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Mwinyi leo tarehe 12 Januari, 2022 ameongoza mamia ya Wazanzibar na Watanzania kusherehekea kilele cha miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu Zanzibar. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea)

Sherehe hizo zimepambwa vilivyo kwa burudani mbalimbali ikiwamo, gwaride kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama nchini sambamba na ngoma za asili kutoka kwa wananchi wa mikoa ya Zanzibar.

Pia zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwamo Rais Samia Suluhu, Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Viongozi wengine ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda na Fredrick Sumaye, Makamu wa Rais mstaafu Dk. Gharib Bilali, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud, Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Katika sherehe hizo zilizofanyika katika Uwanja wa Amaan, pia zilipambwa na maandamano kutoka mikoa mitano ya Zanzibar.

Aidha, akitoa salamu za shukrani katika maadhimisho hayo, Makamu wa Rais wa Pili Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Sherehe hizo za Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdalah amewashukuru viongozi wote kwa kushiriki kikamilifu.

Pia amepongeza hotuba ya Rais Dk. Mwinyi aliyoitoa jana kwa Wazanzibar na kuelekeza kuwa wananchi wa Visiwa hivyo wameendelea kujenga matumaini makubwa kwake kutokana na mipango ambayo ameanza kuitekeleza.

“Hotuba imekuwa chachu kuelekea kwenye matarajio ya Wazanzibar, nakuahidi tutaendelea kukuunga mkono kwa hali na mali kuhakikisha mipango hiyo itafanikiwa ipasavyo,” amesema.

Pamoja na mambo mengine amemshukuru Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwa kumpata ushirikiano katika kuandaa sherehe hizo.

error: Content is protected !!