January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gwajima kukiona, Dk. Slaa kutelekezwa

Spread the love

IKIWA ni siku mbili tangu kutangazwa kwa mshindi wa mbio za Urais 2015, na siku moja tangu John Magufuli kukabidhiwa cheti maalumu cha ushindi watu wanaodaiwa kuwa ni usalama wa Taifa wameanza kuwaandama watu. Anaandika Josephat Isango … (endelea).

Wakizungumza kwa kujiamini, watu hao wanaojidai kuwa maofisa wa usalama walikutwa kwenye hoteli moja iliyopo maeneo ya sinza jijini Dar es salaam.

Maofisa hao walijiapiza kuwa watu waliokuwa vinara wa kuwatukana Usalama wa taifa kwa kipindi kirefu na kusababisha usumbufu sasa watakiona.

Mmoja aliyekuwa akitajwa na wenzake kwa jina la Yusufu alinukuliwa akisema “Gwajima ametutukana sana, sasa tutashughulika naye, lakini Dk Willbrod Slaa ambaye awali alikuwa akitutukana sasa japo yupo upande wetu tutamtelekeza maana hatusaidii tena.

Kuripotiwa habari hizo kunakuja takribani mwezi mmoja na wiki tatu tangu Gwajima alipowaonya maofisa hao kuwa wamekuwa wakitumika vibaya.

Gwajima alisema hayo katika hoteli ya LandMark Septemba 8 mwaka huu alipokuwa akimjibu aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) aliyejitokeza kwa waandishi kudai kuwa kupokelewa kwa Edward Lowassa kwenye Chadema kulimfanya yeye ajiondoe Chadema, madai ambayo Gwajima alisema sio ya kweli na kuweka wazi kuwa Dk Slaa alikuwa anatumiwa vibaya na usalama wa Taifa.

Katika hatua nyingine vijana hao wa Usalama walijiapiza kuwa sasa katibu mkuu huyo hana madhara kwa siasa na ameshindwa kukisaidia Chama cha Mapinduzi (CCM) kuisambaratisha Chadema katika uchaguzi ambao CCM walikuwa wameelemewa.

error: Content is protected !!