Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Gwajima aliamsha dude Kawe, ‘sina njaa’
Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Gwajima aliamsha dude Kawe, ‘sina njaa’

Askofu Josephat Gwajima
Spread the love

ASKOFU Josephat Gwajima, mgombea ubunge katika Jimbo la Kawe kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema alianza kuitumikia Kawe siku nyingi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Amesema, kabla ya kuwa mbunge, tayari wakazi wa Salasala 250 na misikiti saba imeneemeka kwa kuunganishia maji kwa fedha zake mwenyewe.

Na kwamba, kazi ya ubunge anayoimba kutoka kwa wananchi, si ya kuganga njaa bali kuwatumikia wananchi wa jimbo hilo tu.

Akizungumza kwenye kampeni zake katika Kata ya Kawe, mgombea huyo amesema hatosubiri fedha za serikali kufanya maendeleo kwenye jimbo hilo bali ataingia mfukoni kwake.

“Mimi sijaja kufanya kazi hii kuganga njaa” amesema Gwasjima na kuongeza “acha hao wa upande ule ambao wanaomba ubunge kutumia fedha waliyokopa benki.”

Askofu Gwajima amesema, atanunua greda na maroli kwa kutumia fedha zake kwa ajili ya kukarabati barabara za mitaa yote ya jimbo la Kawe.

Ameahidi kununua magari ya wagonjwa ambayo yatahudumia jimbo hilo na kwamba, wapo

wabunge ambao aliwasaidia kununua magari 18 ya namna hiyo  na kuwakabidhi kwa ajili ya majimbo yao.

“Ununuzi wa magari haya kwangu ni jambo dogo sasa,” amesema Askofu Gwajima huku akisisitiza atasambaza magari hayo ndani ya jimbo hilo kwa siku 90 baada ya kuchaguliwa.

Askofu Gwajima alitoa ahadi hizo juzi wakati akizungumza na wanachama wa CCM na wananchi wa Kata ya Kawe alikokuwa anaendelea na mikutano yake ya kampeni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!