June 24, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Gwajima aibuka

Spread the love

 

MCHUNGAJI wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, ameibuka na kutiwa mbaroni na jeshi la polisi, anaandika Faki Sosi.

Mchungaji Gwajima alikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jijini Dar es Salaam leo (Jumatatu), majira ya saa moja asubuhi. Alikuwa akirejea nchini kutokea matibabu nje ya nchi.

Taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo zinasema, Mchungaji Gwajima alikamatwa wakati akijiandaa kuondoka uwanjani hapo. Alipelekwa kwenye kituo kikuu cha polisi cha Kati.

Wakili wa Gwajima, Peter Kibatala amethibitishia mwandishi wa habari hizi kukamatwa na kuhojiwa kwa mchungaji huyo machachari nchini.

Hata hivyo, Kibatala hakusema, sababu zilizosababisha Mchungaji Gwajima kukamatwa na kuhojiwa.

“…ni kweli Gwajima alikamatwa na polisi akiwa uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Baada ya kukamatwa alifikishwa kituo cha polisi cha kati kwa ajili ya mahojiano ameeleza Kibatala.

Anasema, “baada ya kuhojiwa kwa muda mfupi, jeshi la polisi liliamua kumuchia Mchungaji Gwajima, hadi hapo litakapomhitaji.”

Wakati Kibatala akigoma kueleza kilichosababisha jeshi la polisi kumkamata na baadaye kumhoji Mchungaji Gwajima, taarifa za ndani ya jeshi hilo zinasema, kiongozi huyo wa kiroho amekamatwa kutokana na tuhuma za uchochozi.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, Mchungaji Gwajima anatuhumiwa kutoa kali za uchochezi akiwa kanisani kwake, pale alipodai kuwa Rais John Magufuli, anahujumiwa na baadhi ya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na waumini wa kanisa lake  mwezi uliyopita, Mchungaji Gwajima alimtuhumu rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete, kugoma kumuachia uenyekiti wa chama Magufuli.

Akadai kuwa kitendo hicho kinadhoofisha utendaji kazi wa kiongozi huyo mkuu wa serikali na kinasababisha CCM kusheheni mapepo.

Tangu kutoa kauli hiyo, viongozi wajuu wa jeshi la polisi, wamekuwa wakidai kuwa wanamtafuta mchungaji huyo, ingawa baadhi ya watu wanasema, “alichokifanya Gwajima kina mkono wa Ikulu.

error: Content is protected !!