October 18, 2021

Uhuru hauna Mipaka

‘Guest house,’ gesi ya kupikia vyapandisha mfumuko wa bei

Spread the love

 

MFUMUKO wa Bei wa Taifa nchini Tanzania kwa mwaka ulioshia Septemba 2021, umeongezeka kwa asilimia 0.2 hadi kufikia asilimia 4.0, kutoka asilimia 3.8 ilivyokuwa Agosti 2021. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa jana Ijumaa, tarehe 8 Oktoba 2021 na Kaimu Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii, katika Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ruth Minja, akizungumza na wanahabari jijini Dodoma.

Minja alisema, mfumuko wa bei nchini umeongezeka kama ilivytokea katika nchi jirani.

Ambapo Kenya kwa mwaka ulioishia Septemba 2021, umeongezeka hadi asilimia 6.91, kutoka asilimia 6.57 kwa mwaka ulioishia Agosti 2021. Huku mfumuko wa Uganda ukiongezeka hadi kufikia asilimia 2.2 kutoka asilimia 1.9 kwenye kipindi hicho.

Ruth Minja, Mtakwimu Mkuu wa Serikali ofisi ya Taifa ya Takwimu

“Mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioshia mwezi Septemba 2021, umeongezeka kidogo hadi asilimia 4.0, kutoka aislimia 3.8 ilivyokuwa Agosti 2021, hili ni badiliko la asilimia 0.2 ikilinganishwa na nchi jirani kama Kenya na Uganda ambapo mfumuko wa bei umeonegzeka kwa asilimia 0.3 kwa kila nchi,” amesema Minja.

Amesema mfumuko wa bei wa Taifa umechangiwa na kupanda kwa bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula, ikiwemo gesi ya kupikia iliyochangia kwa asilimia 2.7, huduma ya malazi katika nyumba za kulala wageni (Guest House), iliyohangia kwa asilimia 5.7.

Bidhaa nyingine zilizochangia mfumuko huo ni, unga wa ngano (6.8), nyama ya ng’ombe (3.4), maziwa ya unga (9.2), mayai (5.0) na viazi (4.7).

Minja amesema mfumuko huo uko ndani ya lengo la Serikali unaowezesha shughuli za kiuchumi kufanyika.

“Napenda kufanunua kwamba, mfumuko wa bei wa Taifa kwa Septemba 2021 wa asilimia 4.0, bado uko ndani ya lengo la Serikali la muda mfupi na wakati wa kuwa na mfumuko wa bei wa asilimia 5, ambao unawezesha shughuli za kiuchumi kufanyika bila athari,” amesema Minja na kuongeza:

“Hata hivyo, Serikali inafanyia kazi changamoto zinazosababisha bei za bidhaa na huduma kupanda , kwa mafano hivi karibuni imeondoa tozo katika bei za mafuta ya Petroli na kutopandisha bei yake kwa Septemba 2021.”

error: Content is protected !!