MAKOCHA Pep Guardiolla wa Manchester City na Ole Gunner Solskjaer wa Manchester United wamejuimishwa kwenye orodha ya makocha watano kuwania tuzo ya kocha bora wa Ligi Kuu nchini England kwa msimu wa 2020/21. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Orodha hiyo imetolewa hii leo ambapo wadau mbalimbali watapata nafasi ya kupiga kura ya kumchagua kocha bora kwa msimu uliomalizika.

Guardiola amejuimuishwa kwenye kikosi hiko mara baada ya kuiongoza klabu yake ya Manchester City kutwaa taji la Ligi Kuu nchini humo kwa mara ya tatu Katika kipindi cha miaka mitano aliyokaa hapo.
Kwa upande wa kocha wa Manchester United Ole Gunner Solskjaer yeye ameingia kwenye kinyang’anyiro hiko mara baada kuiongoza klabu ya Manchester United kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo.

Makocha hayo wawili walifanikiwa pia kuongoza timu zao kwenye fainali mbili kubwa barani Ulaya kwenye ngazi ya klabu na wote walipoteza.
Guardiola aliingai fainali ya michuano ya kombe la Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya na kupoteza mchezo huo kwa bao 1-0, dhidi ya Chelsea, Solskjaer akiwa na kikosi cha Manchester United walipoteza mchezo wa fainali ya Europa kwa mikwaju ya penati dhidi ya Villarreal.

Makocha wengine waliongia kwenye kinyang’anyiro hiko ni Marcelo Bielsa wa Leeds United, David Moyes wa West Ham United pamoja na Branden Rodgers anayekinoa kikosi cha Leceister City.
Leave a comment