May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Guardiola kocha bora Ligi Kuu England

Pep Guardiolla

Spread the love

 

KOCHA wa klabu ya Manchester City ya England Pep Guardiola amefanikiwa kushinda tuzo ya kuwa kocha bora wa Ligi Kuu nchini England mara baada ya kuwabwaga washindani wake. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Guardiola ameshinda tuzo hiyo maara baada ya kutwaa taji la Ligi Kuu nchini humo akiwa na klabu yake ya Manchester City na kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA)

Katika kinyang’anyiro hiko Guardiola alikuwa akichuana na kocha wa Manchester United Ole Gunner Solskjaer huku wengine ni Marcelo Bielsa wa Leeds United, David Moyes wa West Ham United pamoja na Branden Rodgers anayekinoa kikosi cha Leceister City.

Toka alipofika msimu wa 2016 Guardiola amefanikiwa kuipa Manchester City taji la tatu Katika kipindi cha miaka mitano aliyokaa hapo.

 

 

 

error: Content is protected !!