December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

GSM yamwaga fedha Ligi Kuu, yaingia udhamini wa Bil 2

Spread the love

 

KAMPUNI ya Gsm imeingia mkataba wa miaka miwili wa udhamini mweza wa Ligi Kuu Tanzania Bara na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wenye thamani ya Shilingi 2.1 Bilioni. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Hafla ya utiwaji saini mktaba huo, imefanyika hii leo jijini Dar es Salaam, tarehe 23 Novemba, 2021 kwenye kumbi ya Hotel ya Serena.

Katika hafla hiyo ya utiwaji saini, upande wa Gsm uliwakilishwa na mkurugezni mkuu wa uwekezaji Mhandisi Hesri Said, huku Tff ikiwakilisha na makao wa pili wa Rais Athumani Nyamlani ambao wote kwa pamoja ndio waliokuwa na dhamana ya kutia saini katika karatasi hizo.

Mara baada ya kuingia makubaliano hayo Mhandisi Hersi alisema kuwa mktaba huo utakwenda kunufaisha klabu za Ligi Kuu kwa kuwa hakuna mpira bila fedha.

“Mkataba huu wa miaka miwili na utakuwa na thamani ya Shilingi 2.1 bilioni, mkataba huu utakwenda kuvunufaisha klabu za ligi kuu kwa kuwa hakuna mpira bila fedha.” Alisema Hersi

Kabla kuingia mkataba huo, Gsm ilikuwa ikidhamini klabu tatu kwenye Ligi Kuu kwa msimu huu ambazo ni Yanga, Coastal Union pamoja na Namungo FC.

Hersi aliendelea kusema kuwa wao wameamua kufungua milango ili wengine waje, kwa kuwa waliona ipo sababu ya kuunga mkono michezo kwa vitendo na sio maneno.

“Sisi tunafungua milango kwa wengine kusapoti mpira, tumeiona gharama imekuwa kubwa, Gsm iliona ipo sababu ya kuunga mkono michezo na sio kwa maneno bali kwa vitendo.” alisema Hersi

Kampuni hiyo itakuwa ya tatu kwa msimu huu kudhamini Ligi Kuu, mara baada ya Azam Media kusaini kama mdhamini kwenye haki ya matangazo na kisha Benki ya NBC wakisaini kama mdhamini mkuu wa Ligi.

Kwa upande wa Tff ambao waliwakilishwa na Makamo wa kwanza wa Rais, alisema kuwa pesa hizo zinakwenda kunufaisha klabu na wasingependa kuona timu inafungwa kwa sababu ya njaa.

“Pesa hizi shilingi 2.1 bilioni, zitakwenda kunufaisha klabu, hatutaki timu ifungwe kwa sababu ina njaa” alisema Nyamlani.

error: Content is protected !!