Friday , 29 March 2024
HabariMichezo

GSM wapata pigo

Spread the love

BABA mzazi wa mfanyabiashara maarufu na mfadhiri wa klabu ya Yanga, Ghalib Said Mohammed (GSM), mzee Said Mohamed amefariki Dunia leo Jumanne tarehe 1 Machi 2021, Masaki jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Taarifa za kifo hiko zilitolewa leo asubuhi na Mkurugenzi wa uwekezaji wa kampuni ya GSM, Mhandisi Hersi Said kupitia kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mazishi ya Mzee Said Mohammed yatafanyika hii leo majira ya saa 10 jioni kwenye makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam na swala itaswaliwa kwenye msikiti wa Maamur uliopo Upanga.

Mara baada ya kutokea msiba huo, watu mbalimbali maarufu kupitia mitandao ya kijamii walitoa pole kwa familia ya mfanyabiashara huyo, ambaye hivi karibuni alikuwa nchini Dubai.

Kwa upande wa klabu ya Yanga, nao walitoa salamu zao za pole kwa familia ya mfadhiri wao Ghalib Said kwa msiba huo, kupitia taarifa rasmi waliyoitoa hivi punde.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Makala & UchambuziMichezo

TFF kuamua hatima ya Amrouche

Spread the loveHATIMA ya Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Adel Amrouche kuendelea...

Habari za SiasaMichezo

Matinyi: Dk. Ndumbaro alifanya utani ukaguzi mechi za Yanga, Simba

Spread the loveMsemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi amesema kauli iliyotolewa na...

Michezo

Gethsemane Group Kinondoni (GGK) waachia video ya Bwana Wastahili

Spread the loveWAIMBAJI maarufu nchini kutoka Gethsemane Group Kinondoni (GGK)SDA wameachia video...

BiasharaMichezo

Gamondi kocha bora mwezi Februari, NBC yamjaza manoti

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambae ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!