May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

GSM wamkaribisha Manji Yanga

Yusuf Manji

Spread the love

 

MARA baada ya kurejea nchini kwa mfanya biashara Yusuf Manji na kuibuka kwa hisia kali za mashabiki wa klabu ya Yanga kutaka arejee ndani ya klabu hiyo, wafadhiri wa timu hiyo kwa sasa kampuni ya Gsm wamemkaribisha mwenyekiti huyo wa zamani kwa mikono miwili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Manji alirudi nchini siku tatu zilizopita mara baada ya kuondoka nchini toka mwaka 2018 kutokana na matztizo yake binafsi.

Akiongea na chombo kimoja cha habari Mkurugezni wa uwekezaji wa kampuni ya Gsm ambao ni wadhamini wa klabu ya Yanga, Mhandisi hersi Saidi amesekuwa wanamkaribisha mwenyekiti huyo kwa mikono miwili kutokana na klabu hiyo kuwa na mahitaji mengi kwa sasa.

“Hii itakuwa Baraka kubwa kwetu kama Gsm, kwa sababu ilikuwa tiukiita watu kuisapoti timu, Yanga inamahitaji mengi sana kwa kuwa mapato na matumizi ya klabu hayafaniani ndio maana sisi tuliingia kusapoti hii, akitokea mtu tutafurahi sana.” Alisema Hersi

Mhandisi Hersi Said, Mkurugezni wa uwekezaji Gsm

Aidha kiongozi huyo aliongezea kuwa kama akitokea mtu anataka kuongeza nguvu ndani ya Yanga watampokea kwa mikono miwili.

“Akitokea mtu akisema Gsm nataka niongeze nguvu ya kuisapoti Yanga tutampokea kwa mikono miwili.” Aliongezea kiongozi huyo

Mukoko Tonombe mchezaji wa klabu ya Yanga

Manji ambaye alikuwa Mwenyekiti wa klabu ya Yanga toka mwaka 2012 alipata mafanikio makubwa ikiwemo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara mara tatu mfululizo kuanzia msimu wa 2014 mpaka 2017.

error: Content is protected !!