KAMPUNI ya Uwindaji ya Green Mile imeendelea kuvutana na Waziri wa Maliasili na Utalii Dk. Hamisi Kigwangalla, kwa kile walichodai kuwa wataendelea na shughuli zao. Anaripotia Mwandishi Wetu …(endelea).
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Said Mndeme, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, amesema kuwa hakuna taarifa yoyote ya serikali iliyowafikia kuhusu kufutwa kwa kitalu chao.
“Kuna taarifa zinazagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazomuhusisha Dk. Kigwangalla kuwa amefuta umiliki wa kitalu cha uwindaji wa kitalii cha Lake Natron East, kinachomilikiwa na kampuni ya Green Mile Safari.
“Kampuni inazitafsiri taarifa hizo kuwa ni muendelezo wa mkakati wa kuichafua kampuni ya kuiharibia biashara yake. Kampuni yetu haina taarifa yoyote kutoka Serikalini,” amesema Mndeme.
Amesema kuwa shughuli za uwindaji wa kitalii kwenye kitalu hiko zitaendelea kama kawaida.
Amesema kuwa hawaitambui taarifa hiyo kwa sababu ya kukiuka fungu la 38 la sheria ya wanyamapori ya mwaka 2009.
Amedai kuwa baadhi ya watendaji serikalini wamekuwa wakiwakwamisha kwa maslahi yao binafsi.
Leave a comment