May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Grand P amvisha pete mchumba wake live kwenye TV

Spread the love

 

MWIMBAJI mwenye umbo la mbilikimo kutoka nchini Guinnea, Moussa Kaba maarufu kama Grand P amemvalisha pete mpenzi wake mwenye umbo matata raia wa Ivory Coast na mwanamitindo Eudoxie Yao. Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea)

Tukio hilo lilifanyika live kwenye Televisheni iliyofahamika kwa jina la Life Tv iliyopo huko nchini Ivory Coast wakati wawili hao wakiendelea kuhojiwa.

Aidha, baada ya tukio hilo, mwanadada Eudoxie Yao ambaye ana umbo namba nane linalotafsiriwa kuwatoa udenda vidume wengi Afrika na duniani, aliposti kipande cha video kikikuonesha Grand P akipiga magoti kwenye studio za televisheni hiyo na kumtoa ombi rasmi la ndoa kwa kumvalisha pete hiyo.

Katika video hiyo ambayo Yao ameipakia katika ukurasa wake wa Instagram, Grand P anaonekana akimvisha pete na kutoa ombi hilo kwa lugha ya Kifaransa.

Eudoxie Yao alionekana kufurahia ombi hilo na kumuinua mpenzi wake huyo na katika video hiyo.

Wawili hao ambao walianza kurindima kwenye dimbi la mapenzi kuanzia mwaka 2020 kabla ya kubwagana mwaka jana na miezi michache baadae kurudiani, sasa ni rasmi penzi hilo linaweza kukita mizizi ndani ya ndoa.

Hata hivyo, mwana dada huyo bado ana wasiwasi kwani katika maneno aliyozungumza kwenye tukio hilo alieleza kwambalicha ya kufurahia uamuzi wa Grand P lakini mpenzi wake huyo ana kazi ya kuifanya katika kufikia maamuzi ambayo hatoyajutia mbeleni.

“Pendekezo la ndoa kutoka kwa mpenzi wangu wa zamani lilikuwa la moto kweli kweli, lilikuwa live kwenye runinga. Ni uamuzi mkubwa ameufanya… bado naweza kumuamini kweli Grand P?” aliuliza mwanamitindo huyo.

Wawili hao inadaiwa penzi lao awali liliingia kidudu mtu baada ya Grand P kudaiwa kuchepuka na wanawake tofautitofauti.

Grand P ambaye ana umri wa miaka 32 sasa, amezaliwa na tatizo la kiafya linalofahamika kwa jina la Progeria. Huu ni ugonjwa adimu wa maumbile unamsababisha binadamua kuzeeka mapema.

Hata hivyo, tangu waanze safari yao ya mapenzi, wawili hao wamekuwa kivutio hasa ikizingatiwa maumbile ya Grand P ambaye anaonekana kama mtoto kwa mwanadada huyo.

error: Content is protected !!