July 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Goodluck Jonathan kuwania urais tena

Spread the love

ALIYEKUWA rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan ametangaza kuwania urais wa taifa hilo na kubadili mpango wa awali wa kutowania tena wadhifa huo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Jonathan ni miongoni mwa wanasiasa 26 ambao wametangaza nia yao ya kumrithi Rais Muhammadu Buhari ambaye kipindi chake cha kuhudumu kinakamilika mwaka ujao.

Hivi karibuni Jonathan ameonekana kuwa mwandani wa karibu wa Rais Buhari, amebadili chama chake cha People’s Democratic Party (PDP) na kujiunga na kile cha Rais Buhari cha All Progressives Congress (APC) ambacho kilimuondoa madarakani mwaka 2015.

Wiki iliyopita, Rais Buhari aliagiza mawaziri wote wanaolenga kuwania nyadhifa za kisiasa kujiuzulu kabla ya kufikia Mei 16.

Wengine ambao wametangaza kuwania urais ni pamoja na Makamu rais wa sasa Yemi Osinbajo, mwenyekiti wa chama tawala Ahmed Bola Tinubu, pamoja na waliokuwa mawaziri 13 na magavana.

Wengina wanaowania kupeperusha bendera ya chama cha upinzani cha PDP, ni pamoja na aliyekuwa makamu rais Atiku Abubakar, aliyekuwa spika wa bunge la seneti, Bukola Sarak, gavana wa Sokoto, Aminu Tambuwa na gavana wa jimbo la Rivers, Nysom Wike.

error: Content is protected !!