July 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gomes, Bocco wapeta tuzo mwezi Juni

John Bocco mshambuliaji wa Simba

Spread the love

 

KOCHA wa klabu ya Simba, Didier Gomes pamoja na mshambuliaji wa klabu hiyo John Bocco wameshinda tuzo, mwezi Juni kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Bocco ambaye pia ni nahodha wa kikosi hiko, ameshinda tuzo hiyo mara baada ya kufanya vizuri kwenye michezo ya mwezi Juni.

Katika mwezi Juni Bocco amecheza jumla ya michezo mitatu na kupachika mabao matatu ambapo timu yake iliibuka na ushindi katika michezo hiyo.

Kwenye kinyang’anyiro hiko, Bocco amewashinda wachezaji Feisal Salum wa Yanga, pamoja Iddi Suleiman anayekipiga na Azam FC.

Didier Gomes kocha wa Simba

Hii itakuwa mara ya pili kwa Bocco kutwaa tuzo hiyo, mara ya kwanza kwa msimu huu ilikuwa mwezi Novemba, mwaka jana.

Kwa upande wa kocha Gomes yeye alifanikiwa kunyakuwa tuzo hiyo, mara baada ya kuikngoza Simba kushinda michezo yote mitatu ya mwezi Juni, ambapo aliibuka na ushindi wa mabao 3-0, dhidi ya Ruvu Shooting, pia aliibuka na ushindi wa bao1-0, mbele ya Polisi Tanzania na kisha kuichakaza Mbeya City mabao 4-0.

error: Content is protected !!