August 18, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Goli la mkono lanukia umeya Kinondoni

Casimir Mabina, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani

Spread the love

CASIMIR Mabina, Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Kanda ya Pwani amesema wamejipanga kudhibiti hila za Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinachotaka kutwaa umeya wa Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, kinyume na utaratibu, anaandika Pendo Omary.

Uchaguzi wa Meya wa Manispaa ya Kinondoni utafanyika tena baada ya kugawanywa kwa manispaa hiyo na kupatikana nyingine ya Ubungo, kwa lengo la kuongeza ufanisi ikiwemo kusogeza karibu zaidi huduma kwa wananchi.

Akizungumza na mtandao huu siku ya leo, Mabina amesema CCM inafanya hila za kupunguza madiwani wawili, mmoja kutoka Chadema na mwingine Chama cha Wananchi- CUF katika Manispaa ya Kinondoni huku wakikiongezea chama tawala diwani mmoja ili kutengeneza mazingira ya ushindi usio halali.

“Chadema tuna madiwani 13, CUF 7 na CCM 16 kwahiyo kwa ujumla vyama vya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) tuna madiwani 20 dhidi ya 16 wa chama tawala.

Mkurugenzi wa manispaa anawatafutia ushindi wa kilazima CCM, ameandika barua ya kupunguza madiwani wa upinzani na kuongeza wa CCM. Anataka Chadema tuwe na madiwani 12, CUF 6 na CCM 17 ili pawe na tofauti ya diwani mmoja wakati tulikuwa na tofauti ya madiwani wanne,” amesema Mabina.

Mabina amesema kuwa wakati Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni pia amewaandikia barua ya kuwataka kuwasilisha majina ya madiwani wa viti maalum upya, hatua ambayo inatafsiriwa kama kutaka kutangaza upya majina ya wabunge wa viti maalum na manispaa zao, zoezi ambalo lilishafanyika mwaka jana.

“Mkurugenzi amehamisha wabunge wote wa CCM wa viti maalum na hata wa kuteuliwa na rais wote wametolewa Ubungo na kupelekwa Kinondoni akiwemo Dk. Tulia Ackson ambaye anaishi Jimbo la Kibamba.

“Anasahau kuwa kati ya wabunge hao 5 wa CCM, wawili wa viti maalum na watatu wateule wa rais wamepoteza sifa za kuwa wajumbe wa Baraza la Manispaa ya Kinondoni kwa kushidwa kuhudhiria kikao chochote tangu baraza lilipoundwa kwa kumchagua Meya,” amesema Mabina.

error: Content is protected !!