May 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Giggy Money amaliza kifungo ‘Zanzibar nakuja kivingine’

Gift Stanford 'Giggy Money'

Spread the love

 

MSANII wa muziki wa bongo fleva nchini Tanzania, Gift Stanford maarufu Giggy Money ameahidi mashabiki zake kwamba hatofanya makosa tena kamak kama kipindi cha nyuma na kusababisha kufungiwa miezi sita. Anaripoti Matilda Peter, Dar es Salaam … (endelea).

Giggy Money amemaliza kifungo cha miezi sita kujihusisha na kazi za sanaa ndani na nje ya Tanzania alichopewa tarehe 5 Januari 2021 na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata).

Basata, walimfungia na kumtoza faini ya Sh.1 milioni. Ni baada ya kushiriki katika tamasha la Wasafi ‘Tumewasha Tour’ lililofanyika jijini Dodoma uwanja wa Jamhuri na kupanda jukwaani kwa ajili ya kutumbuiza na kuvua gauni (dela) na kubakia na vazi ambalo lilikuwa linaonyesha maungo yake ya mwili.

Jana Jumatano, tarehe 18 Agosti 2021, Giggy Money akizungumza na MwanaHALISI Online alisema, amejipanga kuanza kutoa burudani kambambe kwa mashabiki zake.

Alisema hayo muda mfupi baada ya hafla ya kupata ubalozi wa saloon ya suzana iliyopo Tegeta mkoani Dar es Salaam.

Msanii huyo amesema, hatovaa mavazi yatakayomwekq nusu utupu, bali atahakikisha anavaa mavazi ya kuvutia na kupendeza kwasababu vazi ni moja ya sanaa pia.

Giggy ni moja kati ya wasanii watakao tumbuiza Zanzibar Jumamosi hii tarehe 21, Agost 2021 katika tamasha la msanii Zuchu kutoka rebo ya WCB.

Aliwahakikishia wakazi wa Zanzibar kuwa watapata burudani ya aina yake siku hiyo na kuwaambia wakae mkao wa kula kuona makubwa ambayo amejiandaa kwa ajili ya siku hiyo kwani anakuja kivingine.

error: Content is protected !!