July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Gianni Infantino Rais mpya wa Fifa

Spread the love

GIANNI Infantino, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Fifa, amechaguliwa kuwa Rais mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (Fifa) katika uchaguzi uliomalizika hivi punde huko Zurich, Uswisi, anaandika Erasto Masalu.

Infantino ambaye ni raia wa Switzerland amemrithi Sepp Blatter baada ya kupata kura 115 katika raundi ya pili ikiwa ni kura 27 zaidi ya mpinzani wake wa karibu Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa.

Mwanamfalme Ali bin al-Hussein alikuwa wa tatu akiwa na kura nne huku Jerome Champagne akishindwa kupata hata kura moja. Tokyo Sexwale raia wa Afrika Kusini alijiondoa kabla ya kura kuanza kupigwa.

Raundi ya kwanza ya upigaji kura ilishindwa kumbaini mshindi wa moja kwa moja, hivyo uchaguzi huo kuingia raundi ya pili ambapo wingi wa kura unaweza kumwezesha mgombea kutangazwa mshindi katika raundi ya pili.

Blatter ambaye aliliongoza shirikisho hilo tangu mwaka 1998 alijiondoa mwaka uliopita kabla ya kupigwa marufuku katika shughuli zozote za kandanda kwa kipindi cha miaka sita .

Baada ya kutangazwa mshindi, Infantino aliwaambia wajumbe waliopiga kura kwamba hakuweza kujielezea kutokana na hisia alizokuwa nazo.

Lakini aliwaambia wajumbe kwamba: ”Kwa pamoja wataweza kuirudisha sura ya Fifa na heshima ya Fifa”.

error: Content is protected !!